Damus
POWA255 profile picture
POWA255
@POWA255

POWA 255 ni mpango wa elimu ya Bitcoin kwa njia ya mtu kwa mtu (peer-to-peer) unaolenga kusambaza maarifa ya Bitcoin kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Relays (6)
  • wss://relay.primal.net – read & write
  • wss://relay.nostr.band – read & write
  • wss://nostr.se7enz.com – read & write
  • wss://atlas.nostr.land – read & write
  • wss://nostr.diakod.com – read & write
  • wss://profiles.nostr1.com – read & write

Recent Notes

POWA255 profile picture
Trezor Academy Session 2/3 Recap ⚡

Tarehe 21/02/2026, @Bitcoin Arusha Bikwa kushirikiana na #powa255 tuliendesha kwa mafanikio Session ya 2/3 ya #TrezorAcademy.

Katika session hii tuliangazia kwa undani:
🔐 Maana na matumizi ya custodial wallets
📤📥 Jinsi ya kutuma na kupokea Bitcoin
🛒 Matumizi ya Bitcoin katika maisha ya kila siku
💳 Namna ya kununua Bitcoin kupitia #Chapsmart

Washiriki walipata uelewa mpana zaidi kuhusu uhifadhi na matumizi sahihi ya Bitcoin kwa vitendo.

Usikose Session ya Mwisho (3/3) itakayofanyika tarehe 28/02/2026 pale pale Bitcoin Arusha Hub.

Karibu ujifunze, ukue na ujijengee uhuru wa kifedha kupitia Bitcoin 🚀

#BitcoinArusha #TrezorAcademy #BitcoinEducation #Powa255

@Man Like Kweks @SatsTagga⚡






2❤️1👁️1
POWA255 profile picture
🎓 TREZOR ACADEMY – TANZANIA 🇹🇿
Bitcoin Education • Self-Custody • Security

🌍 #TrezorAcademy iko katika nchi 28 duniani
✨ Tanzania ni mojawapo!

📅 Mwezi wa Pili (Februari 2026)
Bitcoin Arusha kwa kushirikiana na Powa 255 itaandaa muendelezo wa vipindi 3 vya Trezor Academy:

🗓 Tarehe:
• 14 Februari-BITCOIN NI NINI

• 21 Februari-MATUMIZI YA BITCOIN

• 28 Februari- WATUMIAJI WENGINE WA BITCOIN WANAFANYA NINI?

📍 Mahali:
Bitcoin Arusha Hub Jengo la Mega Complex floor ya Saba/WSHA Co-working space

📝 Jisajiri hapa kwaajiri ya session ya kwanza, Usajiri wa Session ya pili na ya tatu zitafata baada ya session ya kwanza kufanyika

https://luma.com/mzi8z2vd

🏅 Vyeti (Certificates)
🎁 Zawadi mbalimbali
Zitatolewa kwa washiriki watakaohudhuria vipindi vyote vitatu kikamilifu

🤝 Imeandaliwa na: Powa255 x Bitcoin Arusha × Trezor Academy



1❤️1
POWA255 profile picture
Tarehe 23/01/2026, POWA 255 na @Bitcoin Arusha kwa kushirikiana na @Hedhi Huru | Reusable Pads and Bitcoin Education walifanikisha mpango wa Reusable Menstrual Pads.

Katika mpango huu, pedi zinazoweza kutumika tena zilitengenezwa na kugawiwa kwa wanafunzi takribani 42 wa Shule ya Sekondari Manushi, iliyopo Moshi, mkoa wa Kilimanjaro.


♻️📦 Pedi hizi zitawasaidia wanafunzi kuendelea kukaa shuleni kipindi chote cha hedhi kwa hadi miaka mitatu, bila vikwazo wala kukosa masomo.

🤝 Wewe pia unaweza kuwa sehemu ya mabadiliko haya
Support kwa kumnunulia mwanafunzi mfuko mmoja wa pedi kupitia @Geyser

https://geyser.fund/project/hedhihuru/posts/view/5473?mtm_campaign=project-share&mtm_keyword=hedhihuru-post-5473&mtm_source=visitor&mtm_medium=geyser&mtm_content=post-share-button

1
Tracking Token Disrespector · 21w
🤖 Tracking strings detected and removed! 🔗 Clean URL(s): https://geyser.fund/project/hedhihuru/posts/view/5473 ❌ Removed parts: ?mtm_campaign=project-share&mtm_keyword=hedhihuru-post-5473&mtm_source=visitor&mtm_medium=geyser&mtm_content=post-share-button
POWA255 profile picture
Tunafuraha kuwatangazia kuwa tumepokea vitabu viwili vya “THE BITCOIN STANDARD” vilivyotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili kutoka Nairobi Kenya🇰🇪

Shukrani za dhati kwa exonumia.africa kwa kazi yao kubwa ya kutafsiri na kuifanya elimu ya #Bitcoin ipatikane kwa urahisi zaidi na kuwawezesha watu wengi kujifunza kwa lugha yao mama.

Nakala moja ya vitabu hivi itatolewa shuleni ili kusaidia elimu na uelewa wa maswala ya fedha.

Nakala nyingine itabaki katika hub ya @Bitcoin Arusha kwajili ya jamii kusoma, kujifunza na kukua pamoja.

Hii ni hatua kubwa kuelekea kusambaza elimu ya #bitcoin Tanzania na barani Africa kwa ujumla.
#BitcoinNiHela
#bitcoinforeveryone


23❤️6
Noelyne · 22w
Hongera kwa hatua hii! 👏🏾
POWA255 profile picture

Jumamosi tarehe 17/01 tulifanya Banda letu la kwanza la P2P katika Hub ya @Bitcoin Arusha 🇹🇿⚽️

Tuliuangalia derbi ya Man United dhidi ya Man City huku tukiwatambulisha @vexl 😎 katika jamii yetu na kuelezea kwa nini #Bitcoin ya #peer-to-peer ina umuhimu mkubwa.

Tutapanga matukio zaidi ya kijamii ili kuimarisha mitandao ya P2P na kuukuza uchumi wa mzunguko wa #Bitcoin hapa kwetu.
1❤️1
POWA255 profile picture
Kesho tarehe 16 Januari, Bitcoin Arusha inaelekea Moshi kutembelea wanawake wanaotengeneza pedi za #HedhiHuru zinazoweza kutumika tena zikisaidia kuleta heshima, biashara za kienyeji, na athari chanya katika maendeleo ya elimu ya wanafunzi wa kike.💪🏾🧡
2❤️1
POWA255 profile picture
@Hedhi Huru | Reusable Pads and Bitcoin Education inatengeneza taulo za kike zinazoweza kutumika tena na tena kwajili ya kuwasaidia mabinti hapa Tanzania kuhudhuria Masomo Yao bila vikwazo Wakati wa hedhi.

Kwa shilling elfu sabini na tano tu (Sawa na $30) unaweza kumsaidia binti mmoja kupata taulo hizi kwa matumizi ya miaka mitatu mfululizo.

Ni nafasi ya wewe kuwa sehemu ya mabadiriko. Kila mchango wako ni uwekezaji katika elimu na heshima ya msichana!!!!!
#BitcoinForChange⚡️
1