Damus
BITCOINSAFARITZ profile picture
BITCOINSAFARITZ
FAHAMU KWA HARAKA

Bitcoin Dominance ni nini na kwa nini Altcoins hushindwa kupanda wakati Bitcoin inapanda?

1. Bitcoin Dominance ni nini?
Bitcoin Dominance (BTC.D) ni asilimia (%) inayoonyesha ni kiasi gani cha pesa zote za crypto kipo kwenye Bitcoin.
👉 Kwa maneno rahisi:
Bitcoin Dominance = Sehemu ya soko lote la crypto inayochukuliwa na Bitcoin.
_Mfano:_
Soko lote la crypto = trilioni 1
Bitcoin peke yake = trilioni 0.6
Bitcoin Dominance = 60%
Hii ina maana:
Kila shilingi 10 za crypto, shilingi 6 zipo kwenye Bitcoin.

2. Kwa nini Bitcoin Dominance ni muhimu?
Kwa sababu inaonyesha pesa zinaelekea wapi:
Zinaenda kwenye Bitcoin?
Au zinaenda kwenye Altcoins?
Crypto market ni kama mtiririko wa maji:
Maji yakimiminika kuelekea Bitcoin - Altcoins hukauka
Maji yakitoka kwa Bitcoin - Altcoins huchanua

3. Historia fupi (Muhimu sana kuelewa)

Mwanzoni (2010–2014)
Bitcoin ilikuwa karibu 100%
Hakukuwa na altcoins nyingi

2017 (ICO Boom)
Altcoins nyingi zilitokea
Bitcoin dominance ilishuka sana
Altcoins zilipanda kwa fujo 👉 Altcoin Season

2018–2019 (Bear Market)
Soko lilianguka
Watu wakarudi kwenye Bitcoin ambayo ni salama zaidi
Bitcoin dominance ikapanda tena

2020–2021 (DeFi & NFTs)
Altcoins mpya zikalipuka
Bitcoin dominance ikashuka tena

FUNZO:
Bitcoin huongoza kwanza, altcoins hufuata baadaye.

4. Uhusiano kati ya Bitcoin Dominance na Altcoins
Hapa ndipo watu wengi wanachanganyikiwa 👇

_Bitcoin Dominance ikipanda_
- Pesa zinahamia Bitcoin
- Altcoins hazipandi au zinashuka
Hata kama altcoin inapanda kwa USD, inaweza kushuka ukilinganisha na BTC
👉 Hii ni Bitcoin Season

_Bitcoin Dominance ikishuka_
- Pesa zinahama kutoka Bitcoin
- Zinaingia kwenye altcoins
Altcoins zinaanza kupanda kwa kasi
👉 Hii ni Altcoin Season

5. Kwa nini pesa huanza Bitcoin kwanza?
Sababu 4 kuu:
1. Bitcoin ina liquidity kubwa.Rahisi kununua na kuuza
2. Bitcoin inaonekana salama zaidi. Ndiyo “king” wa crypto
3.Taasisi & whales huanza na Bitcoin
Hawaanzi na meme coins
4. Altcoins zina hatari & volatility kubwa. Watu huziingia wakishapata confidence
_Mfano wa maisha:_
Ukipata mshahara:
Kodi kwanza (Bitcoin)
Chakula (Ethereum)
Starehe (Altcoins ndogo)

6.Makosa makubwa traders hufanya
- “Bitcoin inapanda, basi altcoin yangu itapanda”
- Kununua altcoin kwa sababu “imeshashuka sana”
- Kuingia futures bila kuangalia BTC dominance
- Kukosa subira ya market cycles
👉 Market haifanyi kazi kwa huruma.

7. Jinsi ya kutumia Bitcoin Dominance kama trader
Angalia vitu 3: 1.Bitcoin Dominance chart (BTC.D) 2. Bitcoin price 3. Altcoin market cap (TOTAL2)

Scenarios muhimu:
BTC inapanda + Dominance inapanda
👉 Shikilia Bitcoin

BTC imetulia ina tembea sideways + Dominance inashuka
👉 Altcoins zinaanza
BTC inashuka vibaya
👉 Kila kitu ni hatari

8. Dalili za Altcoin Season kuanza
Usikimbilie, subiri hizi ishara:
- Bitcoin dominance inaanza kushuka
- Bitcoin price haipandi sana (range)
- Ethereum inaanza kumpita Bitcoin
- Altcoins nyingi zinaanza kupanda kwa pamoja
👉 Altcoin season haiji kwa kelele, inakuja utaratibu.

9. Limitations
-Bitcoin dominance si indicator pekee
-Stablecoins huathiri market cap
-Fanya risk management usipende kujiaminisha sana kwenye jambo lolote duniani,hutaamini macho yako😀

HITIMISHO
Bitcoin Dominance inakuonyesha wapi pesa zinaenda,sio wapi ndoto zako zinataka ziende.
_Trader mzuri:_
- Hasikilizi hype
- Anaelewa cycles
- Anajua kusubiri

👉 Nasema tena fanya Risk Management kwa kila jambo ufanyalo,la sivyo linaweza kukuta jambo usiamini😀.Nimemaliza