FAHAMU KWA HARAKA
Bitcoin Dominance ni nini na kwa nini Altcoins hushindwa kupanda wakati Bitcoin inapanda?
1. Bitcoin Dominance ni nini?
Bitcoin Dominance (BTC.D) ni asilimia (%) inayoonyesha ni kiasi gani cha pesa zote za crypto kipo kwenye Bitcoin.
π Kwa maneno rahisi:
Bitcoin Dominance = Sehemu ya soko lote la crypto inayochukuliwa na Bitcoin.
_Mfano:_
Soko lote la crypto = trilioni 1
Bitcoin peke yake = trilioni 0.6
Bitcoin Dominance = 60%
Hii ina maana:
Kila shilingi 10 za crypto, shilingi 6 zipo kwenye Bitcoin.
2. Kwa nini Bitcoin Dominance ni muhimu?
Kwa sababu inaonyesha pesa zinaelekea wapi:
Zinaenda kwenye Bitcoin?
Au zinaenda kwenye Altcoins?
Crypto market ni kama mtiririko wa maji:
Maji yakimiminika kuelekea Bitcoin - Altcoins hukauka
Maji yakitoka kwa Bitcoin - Altcoins huchanua
3. Historia fupi (Muhimu sana kuelewa)
Mwanzoni (2010β2014)
Bitcoin ilikuwa karibu 100%
Hakukuwa na altcoins nyingi
2017 (ICO Boom)
Altcoins nyingi zilitokea
Bitcoin dominance ilishuka sana
Altcoins zilipanda kwa fujo π Altcoin Season
2018β2019 (Bear Market)
Soko lilianguka
Watu wakarudi kwenye Bitcoin ambayo ni salama zaidi
Bitcoin dominance ikapanda tena
2020β2021 (DeFi & NFTs)
Altcoins mpya zikalipuka
Bitcoin dominance ikashuka tena
FUNZO:
Bitcoin huongoza kwanza, altcoins hufuata baadaye.
4. Uhusiano kati ya Bitcoin Dominance na Altcoins
Hapa ndipo watu wengi wanachanganyikiwa π
_Bitcoin Dominance ikipanda_
- Pesa zinahamia Bitcoin
- Altcoins hazipandi au zinashuka
Hata kama altcoin inapanda kwa USD, inaweza kushuka ukilinganisha na BTC
π Hii ni Bitcoin Season
_Bitcoin Dominance ikishuka_
- Pesa zinahama kutoka Bitcoin
- Zinaingia kwenye altcoins
Altcoins zinaanza kupanda kwa kasi
π Hii ni Altcoin Season
5. Kwa nini pesa huanza Bitcoin kwanza?
Sababu 4 kuu:
1. Bitcoin ina liquidity kubwa.Rahisi kununua na kuuza
2. Bitcoin inaonekana salama zaidi. Ndiyo βkingβ wa crypto
3.Taasisi & whales huanza na Bitcoin
Hawaanzi na meme coins
4. Altcoins zina hatari & volatility kubwa. Watu huziingia wakishapata confidence
_Mfano wa maisha:_
Ukipata mshahara:
Kodi kwanza (Bitcoin)
Chakula (Ethereum)
Starehe (Altcoins ndogo)
6.Makosa makubwa traders hufanya
- βBitcoin inapanda, basi altcoin yangu itapandaβ
- Kununua altcoin kwa sababu βimeshashuka sanaβ
- Kuingia futures bila kuangalia BTC dominance
- Kukosa subira ya market cycles
π Market haifanyi kazi kwa huruma.
7. Jinsi ya kutumia Bitcoin Dominance kama trader
Angalia vitu 3: 1.Bitcoin Dominance chart (BTC.D) 2. Bitcoin price 3. Altcoin market cap (TOTAL2)
Scenarios muhimu:
BTC inapanda + Dominance inapanda
π Shikilia Bitcoin
BTC imetulia ina tembea sideways + Dominance inashuka
π Altcoins zinaanza
BTC inashuka vibaya
π Kila kitu ni hatari
8. Dalili za Altcoin Season kuanza
Usikimbilie, subiri hizi ishara:
- Bitcoin dominance inaanza kushuka
- Bitcoin price haipandi sana (range)
- Ethereum inaanza kumpita Bitcoin
- Altcoins nyingi zinaanza kupanda kwa pamoja
π Altcoin season haiji kwa kelele, inakuja utaratibu.
9. Limitations
-Bitcoin dominance si indicator pekee
-Stablecoins huathiri market cap
-Fanya risk management usipende kujiaminisha sana kwenye jambo lolote duniani,hutaamini macho yakoπ
HITIMISHO
Bitcoin Dominance inakuonyesha wapi pesa zinaenda,sio wapi ndoto zako zinataka ziende.
_Trader mzuri:_
- Hasikilizi hype
- Anaelewa cycles
- Anajua kusubiri
π Nasema tena fanya Risk Management kwa kila jambo ufanyalo,la sivyo linaweza kukuta jambo usiaminiπ.Nimemaliza
