Happy Bitcoin Birthday! ๐๐งก โ Genesis Block Day Special Recap from Arusha
Januari 3 ni siku muhimu sana kwenye historia ya Bitcoin siku tunayoenzi kama Genesis Block Day, siku ambayo block ya kwanza ya Bitcoin (Genesis Block) ilichimbwa na muanzilishi wa Bitcoin, Satoshi Nakamoto, mwaka 2009. Siku hii inaashiria kuzaliwa kwa mfumo wa fedha wa kidijitali usio na udhibiti wa kati Bitcoin. Ndani ya block hiyo ya kwanza kulikuwa na ujumbe maarufu kutoka gazeti la The Times uliosomeka: "Chancellor on brink of second bailout for banks," ukitoa ujumbe wa wazi juu ya sababu za kuzaliwa kwa Bitcoin: kuleta mabadiliko katika mfumo wa kifedha wa kidunia.
Katika kusherehekea siku hii ya kihistoria, Bitcoin Arusha Community waliandaa Genesis Block Day Hangout hapo jana, katika Westerwelle Startup Haus Arusha. Tukio hili lilikusanya vijana mbalimbali kutoka maeneo tofauti kuzungumza, kujifunza, na kubadilishana uzoefu juu ya Bitcoin na teknolojia ya blockchain.
Tukio lilijumuisha mijadala juu ya:
- Elimu ya msingi kuhusu Bitcoin na Lightning Network
- Fursa zinazopatikana ndani ya sekta hii ya teknolojia
- Njia bora na rahisi za kuanza kujifunza
- Ujumuishaji wa jamii kupitia teknolojia huru
- Networking na washiriki wa Bitcoin ecosystem kutoka ndani na nje ya Arusha
Ilikuwa siku ya pekee sana yenye maarifa, hamasa, na maono makubwa ya kuendeleza ujumuishaji wa kijamii na kiuchumi kupitia Bitcoin.
Tunawapongeza sana Bitcoin Arusha, ManLikeKweks, Satstags, na timu nzima kwa kuandaa tukio hili zuri. Pia ilikuwa furaha kubwa kukutana na Bitcoiners kama Jacob, Chapsmart.com, Hussein, Graysatoshi na wengine wengi waliokuja kushiriki.
Tunaendelea kusambaza elimu, hamasa, na ujumi wa Bitcoin kote Afrika!
#GenesisBlockDay #BitcoinArusha #BitcoinTanzania #BitcoinEducation