Tunafuraha kuwatangazia kuwa tumepokea vitabu viwili vya “THE BITCOIN STANDARD” vilivyotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili kutoka Nairobi Kenya🇰🇪
Shukrani za dhati kwa exonumia.africa kwa kazi yao kubwa ya kutafsiri na kuifanya elimu ya
#Bitcoin ipatikane kwa urahisi zaidi na kuwawezesha watu wengi kujifunza kwa lugha yao mama.
Nakala moja ya vitabu hivi itatolewa shuleni ili kusaidia elimu na uelewa wa maswala ya fedha.
Nakala nyingine itabaki katika hub ya
@nprofile1q... kwajili ya jamii kusoma, kujifunza na kukua pamoja.
Hii ni hatua kubwa kuelekea kusambaza elimu ya
#bitcoin Tanzania na barani Africa kwa ujumla.
#BitcoinNiHela#bitcoinforeveryone

